Saturday, May 16, 2015

Tangazo la Kuitwa Kazini ( Serikalini)....Limetolewa Tarehe 15 May 2015


Kumb. Na. EA.7/96/01/H/                                                                               15 Mei, 2015

KUITWA KAZINI

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kuanzia tarehe 27/03/2015 hadi tarehe 01/04/2015 kuwa mchakato wa kuwapangia vituo vya kazi umekamilishwa. 
 
Orodha ya majina ya waliopangiwa vituo vya kazi ni kama yanavyoonekana katika Tangazo hili. 
 
Orodha hii pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Data base) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.
 
Aidha, wanatakiwa kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa katika muda ambao umeainishwa kwenye barua zao za kupangiwa vituo vya kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira.
 
Barua za kuwapangia vituo vya kazi zimetumwa kupitia anuani zao. Aidha, wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.

******DOWNLOAD THE ATTACHMENT BELOW*****

TANGAZO LA KUITWA KAZINI SERIKALINI
advert
Share your thoughts using below comment form!