Saturday, May 16, 2015

Tangazo la kuitwa kwenye usaili utakaonza tarehe 25 -05-2015


Kumb. Na. EA.7/96/01/H/50                         16 Mei, 2015

 KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika  Utumishi wa Umma kwa niaba Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala za Serikali (MDAs) anatarajia kuendesha usaili na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi, waombaji kazi watakaofaulu usaili. 
 
Wasailiwa walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia yafuatayo: 
 
1. Ukaguzi  wa  vyeti  utafanyika  saa 1:00 kabla  ya  muda  wa  mtihani  wa mchujo kuanza. 
 
2.Usaili utaanza saa moja na nusu asubuhi (1:30) na utafanyika mahali na tarehe kama inavyoonesha katika nafasi husika. 
 
3. Kuja na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi mfano: kitambulisho cha mkazi, kupigia kura, kazi, hati ya kusafirian.k
4. Kuja  na  Vyeti  Halisi (original certificates) vya  kuanzia  kidato cha nne, sita, Stashahada,Stashahada  ya  Juu, Shahada  na  kuendelea kutegemeana na sifa za mwombaji. 
 
5. “Testmonials”,  “Provisional Results”, “Statement of results”, hatimatokeo  za  kidato cha nne  na  sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA. 
 
6. Kila msailiwa aje na picha moja (Passport size).
7.Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi. 
 
8.Kila msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa kufanyiwa usaili
 
9.Kila  msailiwa  aje  na  cheti  halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate) 

10.Kwa  wale waliosoma  nje  ya Tanzania wahakikishe  vyeti  vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU & NECTA)
 
11.Wale  ambao  majina  yao  hayakuonekana  katika  tangazo  hili watambue  kuwa  maombi  yao  hayakufanikiwa  na  wasisite  kuomba tena mara nafasi za kazi zitakapotangazwa.

******DOWNLOAD THE ATTACHMENT BELOW*****
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
advert
Share your thoughts using below comment form!