Friday, May 15, 2015

Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi- Mwanza...Mwisho Tarehe 30 May 2015


MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MISUNGWI ANAWATANGAZIA WANANCHI NAFASI ZA KAZI MBALIMBALI KAMA IFUATAVYO
===============
 
1. AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA II (V.E.O II) – TGS C- NAFASI 48

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa kwa waliohitumu kidato cha IV au VI na waliohitimu stashahada au shahada ya juu, Uongozi, Maendeleo ya jamii, kilimo, sheria kutoka vyuo vinavyotambulika na serikali

2. AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III TGS A/B- NAFASI 1

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa kwa waliohitumu kidato cha IV au VI na waliohitimu Astashahada ya maendeleo ya Jamii, sheria, Mipango ya Maendeleo vijijini  kutoka vyuo vinavyotambulika na serikali
3. KATIBU MUHTASI (PERSONAL SECRETARY II ) -NAFASI – 2 (TGS C)
 
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa kwa waliohitumu kidato cha IV, waliohudhuria mafunzo ya Uhazili kutoka katika chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) au vyuo vinavyotambuliwa na serikali na kufaulu mitihani ya hatua ya tatu somo la Hati mkato ya Kiswahili na Hati makato ya Kiingereza maneno 80 kwa dakika na mafunzo ya kompyuta na kupata cheti katika program za WINDOWS, MICROSOFT OFFICE, INTERNET, E-MAIL NA PUBLISHER

4. DEREVA DARAJA LA II- TGS A – NAFASI 1
 
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye cheti cha mtihani wa kidato cha IV wenye leseni daraja C ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari  kwa muda usiopungua miaka (3) bila kusababisha ajali, wenye cheti cha majaribio ya ufundi Daraja II
 
JINSI YA KUTUMA MAOMBI
Maombi yote yatumwe kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kwa anuani ifuatayo:
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
S.L.P 20
MISUNGWI
 
MASHARTI YA JUMLA
  1.  Awe raia wa Tanzania
  2. Awe mwenye maadili mazuri
  3. Hajafukuzwa kazi
  4. Hajapunguzwa kazi
  5. Hajafungwa na kupatikana na kosa la jinai
  6. Awe tayari kufanya kazi eneo lolote Misungwi bila kuhama kwa kipindi cha miaka 5
  7. Barua ya maombi iambatanishwe na picha (2) za sasa passport size na vivuli (photocopy) vya vyeti vya elimu na Taaluma
  8. Andika namba ya simu ya mkononi katika barua ya maombi ili kurahisisha mawasiliano
Mwisho wa kupokea maombi ni 30/05/2015 saa 9:00 alasiri
 
SOURCE;  MAJIRA 12TH MAY 2015
==========
advert
Share your thoughts using below comment form!