Friday, October 16, 2015

IPTL Wamshitaki tena Kafulila....Wamdai Fidia ya Mamilioni


Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL/PAP Harbinder Singh Seth, amefungua mashtaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu dhidi ya mbunge aliyemaliza muda wake (Kigoma Kusini) kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi David Kafulila.

Katika kesi hiyo iliyofunguliwa na Mwanasheria wa kampuni hiyo Augustine Kusalika, mlalamikaji anaiomba Mahakama imuamuru Kafulila kuilipa IPTL shilingi milioni 100/= kutokana na kuwafungulia mashtaka ambayo yalishindwa kuthibitishwa kuwa IPTL ilitumia njia za udanganyifu kujipatia fedha kutoka kwenye akaunti ya Tegeta-Escrow.

Mwanasheria huyo amesema kuwa katika matukio mbalimbali, ndani na nje ya bunge, Kafulila alitoa madai yaliyokuwa na tafsiri ya wizi dhidi ya PAP na mmiliki wake Harbinder Sigh Seth.
 
 Aidha, katika madai hayo pia Kafulila anatakiwa kumlipa mlalamikaji thamani ya fedha sawa na usumbufu alioisababishia kampuni hiyo pamoja na fidia kwa athari za kibiashara zilizosababishwa na madai hayo ikiwemo kuchafuliwa jina lake na kampuni ya IPTL/PAP.
advert
Share your thoughts using below comment form!