Friday, October 16, 2015

LHRC yatiwa shaka na kauli ya Rais Kikwete


Siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kuonya kutumia nguvu dhidi ya watu watakaokaa umbali wa mita 200 baada ya kupiga kura, wakosoaji wanasema kiongozi huyo anayemaliza muda wake anavuka mipaka.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu (LHRC), Helen Kidjo Bisimba, anasema madai ya wananchi kukaa vituoni kulinda kura zao yanatokana na kupoteza kwao imani na uadilifu wa taasisi zinazotakiwa kusimamia haki na sheria za uchaguzi.
advert
Share your thoughts using below comment form!