Friday, October 16, 2015

Linnah: Mpenzi wangu hataki picha za mitandaoni

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Estelina Sanga ‘Linnah’ amefafanua kwamba haweki picha za mpenzi wake kwenye kurasa zake za mitandaoni kwa kuwa mpenzi wake huyo hataki na si kwamba wameachana.
 
Linnah alieleza kwamba yeye na mpenzi wake huyo raia wa Uganda, Williams Bugeme, wamekubaliana waache utaratibu huo wa kuweka picha zao kwenye mitandao ya kijamii na si kwamba wameachana kama wengi wanavyodhani.
 
“Bado nipo na Williams, wengi wameshangaa kwa nini siku hizi siweki picha nikiwa naye kama nilivyokuwa nafanya hapo zamani, penzi letu bado lipo imara, lakini tumekubaliana tu kwamba tuache kuyaweka hadharani mapenzi yetu,” alisema Linnah.
advert
Share your thoughts using below comment form!