Friday, October 16, 2015

UKAWA yampoteza mwenyekiti mwenza


Mwenyekiti wa chama cha National League for Democracy na pia mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi Tanzania (UKAWA), Emanuel Makaidi, amefariki dunia akitibiwa mkoani Lindi .
 
NLD ni mojawapo ya vyama vinne vya upinzani vinavyounda muungano wa UKAWA, ambao umemsimamisha mgombea mmoja wa urais katika uchaguzi wa Oktoba 25.
 
Makaidi, aliyejizolea umaarufu kwenye umoja huo wa upinzani kama mwanadiplomasia na msuluhishi wa migogoro, amefariki dunia kwa ugonjwa wa moyo.
advert
Share your thoughts using below comment form!